Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’,...
Mshiriki wa shindano la Big Brother
Africa ‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya
waathirika wa dawa za kulevya.
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha
100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa
muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa
kuacha.
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu
mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pee
pressure na watu niokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi…ni yale
maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.
Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana
na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo
amepunguza idadi.
“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku.”
Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu
wenye kibali cha kuvuta bangi katika jimbo la California kwa maelezo ya
daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.
Source: http://www.timesfm.co.tz/