post-feature-image
HomeBurudani

Martha John ndie Redds Miss Iringa 2014

Martha  John katikati akiwa na  washindi  wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya kutanga...


Martha  John katikati akiwa na  washindi  wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya kutangazwa mshindi wa taji la Redds Miss Iringa 2014 jana  katika ukumbi wa St Dominic huku mshindi wa  pili ni Elizabeth Titus na mshindi  wa tatu ni Fowe Mkuchu(picha na Francis Godwin)
………………………………………………….……………..
Na Francis Godwin blog, Iringa
 
MREMBO Martha  John kuuwakilisha mkoa  wa Iringa katika mashindano ya Redds Miss kanda ya nyanda  za  juu kusini baada ya kufanikiwa  kutwaa taji la Redds Miss Iringa 2014 baada ya  kuwashinda washiriki  wenzake nane  waliojitosa katika  kinyang’anyiro  hicho .
 
Martha alitawazwa  kuwa mrembo  wa mkoa  wa Iringa jana  usiku katika ukumbi wa St Dominic shindano  lililoshuhudia na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita .
 
Kutokana na ushindi  huo Martha kwa  sasa  ndie atakayeuwakilisha  mkoa wa Iringa katika  shindano la kumsaka Redds Miss Kanda ya  nyanda za juu  ,onyesho  linalotarajia  kufanyika  ijumaa ya  wiki ijayo mjini Iringa.
 
Jaji  mkuu  wa  shindano hilo Dosi Magambo  mbali ya  kumtangaza Martha  kuwa mshindi  wa kwanza katika kinyang’anyiro  hicho pia  alimtangaza  mshindi wa  pili kuwa ni   Elizabeth Titus na mshindi  wa tatu ni Fowe Mkuchu
 
Akikabidhi  zawadi kwa  washindi  hao kaimu mkuu wa mkoa  wa Iringa Bw Guninita  alisema kuwa  ni imani yake na ya  serikali ya Rais Dr Jakaya  Kikwete  kuona wasanii na washiriki wa  michezo mbali mbali  wanaendelea  kufanya  vema katika nafasi  zao  ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika sanaa mbali mbali.
 
Guninita  alisema  kuwa  mrembo  huyo ambae ameshinda  taji hilo ni lazima  kuendelea  kufanya vema katika  shindano la kanda  na katika  shindano la Taifa  kama  sehemu ya  kuuwezesha  mkoa  wa Iringa kufanya  vema zaidi na ikiwezekana Redds  Miss Tamzania kutoka  mkoa  wa Iringa.
 
Awali  Redds Miss Iringa 2013 Neema Mality alimtaka  mrithi  wake kujitahidi  kujiheshimu na  kutunza  heshima ya taji hilo .
 
Shindano  hilo  lililoandaliwa na kituo  cha Radio Nuru Fm  chini ya uratibu wa Victor Chakudika  washiriki  wote  walipewa  kifuta  jasho cha Sh. 100,000 wakati mshindi wa kwanza alizawadiwa kiasi  cha Tsh 500,000 , mshindi wa pili Tsh 300,000 na mshindi wa tatu  aliambulia  kiasi cha Tsh 200,000
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: Martha John ndie Redds Miss Iringa 2014
Martha John ndie Redds Miss Iringa 2014
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/06/IMG_3895.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/06/martha-john-ndie-redds-miss-iringa-2014.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/06/martha-john-ndie-redds-miss-iringa-2014.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago