…waibuka na wimbo mkali “Ayaya” DIANA Semhando na Zawia ambao ni ...
DIANA Semhando na Zawia ambao ni mastaa wa kundi maarufu la
minenguo Khanga Moja (ambao majuzi walipata msukosuko wa kufyatuliwa
risasi mtaani), wamepata lebo na studio ya Fire Music ya jijini Dar es
Salaam na kupakua wimbo unaokwenda kwa jina la “Ayaya” ambao
utawatambulisha katika ulimwengu mwingine wa sanaa – ulimwengu wa
uimbaji.
Mkurugenzi
mtendaji wa Fire Music, Masoud Kandoro, amesema kuwa wimbo
huo upo katika hatua za mwisho na kwamba wakali hao ambao
watajitambulisha kama WADADA WAWILI wameutendea haki wimbo huo.
“Ni
wimbo mkali, Wadada Wawili wameimba vizuri na kilichobakia ni mambo
madogo madogo, tunataraji kupata rap fupi fupi za Msafiri Diuof ili
kuunogesha zaidi,” alisema Kandoro.
Wimbo
huo umetungwa na kupangiliwa sauti na H- Mbizo ambako ndani yake
utakutana na mistari kama “Penye miti hakutaki wajenzi, panataka
wakwezi”, “Dukani kumejaa vipodozi kuzaa kunataka malezi”, “Taarab
hainogi mapozi inanoga mashauzi”.
H- Mbizo ndiye aliyetunga wimbo wa “Majanga” uliompatika sifa kibao mwanadada Snura.