Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabud...
Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba
anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama
Mungu na watu wa jamii yake.
Arshid Ali Khan, mwenye miaka 13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake
kutokana na mkia huo ingawa unamfanya aonekana kama alama ya uponyaji
katika Jimbo la Punjab, India.
Mtoto huyo anayetumia kiti cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.
Khan anasema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni
Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa
kweli.
Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa tu.
Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake
wawili baada ya baba yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita na mama
yake kuolewa tena.