Pichani ni Wapenzi wa Castle Lite toka sehemu mbalimbali ...
Pichani ni Wapenzi wa Castle Lite toka
sehemu mbalimbali wakipozi katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili
Chaf-Pozi, Soweto.
Hatimaye Bia ya Castle Lite iliwapeleka
mashabiki wanane nchini Afrika Kusini kushuhudia tamasha la mwanamuziki
Timbaland lililofanyika Super Sport Park, Pretoria. Mashabiki hao
waliopatikana mara baada ya kushiriki shindano maalum ambalo liliwataka
kutuma namba zilizokuwa ndani ya vizibo vya bia hiyo na baadae
kuchezeshwa bahati nasibu iliyochagua washindi. Wakiwa nchini Afrika
Kusini mashabiki hao waliweza kutembelea sehemu mbalimbali ikiwa ni
pamoja na Soweto pia maeneo ya jiji la Pretoria kabla ya kuhudhuria
tamasha hilo lililofana
Picha Zaidi Bofya Hapa