Ugonjwa wa kuanguka na kupiga kelele unaowakumba baadhi ya wasichana katika shule mbalimbali nchini, umetajwa kusababishwa n...
Ugonjwa wa
kuanguka na kupiga kelele unaowakumba baadhi ya
wasichana katika shule mbalimbali nchini, umetajwa kusababishwa na
maambukizi ya hofu inayosababisha mwili kupata dalili za magonjwa
yasiyokuwepo.
Mtaalamu wa
saikolojia na theolojia, Mchungaji John
Rowse kutoka taasisi ya The Uhakika
Christian Education Trust Fund kutoka Mbeya, alisema hayo hivi karibuni baada
ya kutembelea shule zinazopata tatizo
hilo mara kwa mara na kuzungumza na wazazi, wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Alisema kuna mambo kadhaa yanayochangia kujenga hofu
hiyo ambayo mwili hujitayarisha kuambukizwa, ikiwemo vitisho vya maisha kwa
wanafunzi vinavyotokana na mambo mbalimbali kama vile ugomvi na mabadiliko
ambapo miili yao inahangaika kujihami.
Kwa mujibu wa Mchungaji huyo, upo uwezekano kuwa
baadhi ya wanaoanguka, ni wasichana
wanaonyanyaswa nyumbani, wengine wanafundishwa kujidharau na wengine
wanabaguliwa na kufanyiwa unyanyapaa shuleni.
Sababu nyingine ya kuanguka kwa wasichana shuleni
kwa mujibu wa Mchungaji Rowse, ni ENDELEA KWA KUBOFYA HAPA