Mpaka sasa zaidi ya asilimia 90 ya maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa sasa hivi ni muda wa kujua washindi wa vip...
Mpaka
sasa zaidi ya asilimia 90 ya maandalizi yote yamekamilika na
kinachosubiriwa sasa hivi ni muda wa kujua washindi wa vipengele
mbalimbali wanavyoshindanishwa kupitia MTV Africa Music Award ‘MAMA’ na
Tanzania upande wa muziki tunae Diamond Platnumz pekee.
Hizi ni picha 10 za Diamond zikimuonyesha akiwa katika maandalizi ya
mwisho ikiwa ni pamoja na interview kadhaa alizofanya kabla ya tuzo
kuanza kutolewa,kama una Dstv tuzo hizi utazishuhudia kupitia channel
322.
Marlon Wayans ambaye ni miongoni mwa Waigizaji na pia mchekeshaji
maarufu nchini Marekani ambaye ni mwandishi wa muswada na mwongozaji wa
filamu,anatarajiwa kuwa ndiye muongozaji upande wa jukwaa katika
ugawaji wa Tuzo hizi.
Sehemu ambayo zitatolewa tuzo hizi ni kwenye Ukumbi wa Durbun
International Convertion Center (ICC) katika mji wa Kwazulu-Natal,
Afrika Kusini,Ripota wako wa nguvu asiyekubali upitwe na kitu chochote
iwe usiku au mchana yuko South Africa kwa ajili ya kukufahamisha kila
kitakachoendelea.