KLABU ya Yanga, jana usiku ilitarajiwa kumsainisha kiungo wa Taifa Stars, Said Juma. Inadaiwa kuwa, aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans van De...
Inadaiwa kuwa, aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ndiye aliyetoa mapendekezo ya kusajiliwa kwa kiungo huyo.
Jana usiku, Yanga ilitarajiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili
lakini kama ingeshindikana jana, basi anaweza akasajiliwa ndani ya siku
mbili kuanzia leo.
Juma aliingia kwenye kikosi cha Taifa Stars hivi karibuni baada ya
kupita kwenye kundi la wachezaji wa kuboresha kikosi hicho, lakini
aliondolewa na kocha mkuu wa timu hiyo, Martius Nooj na jana hakuwepo
uwanjani.
Taarifa ambazo zilipatikana jana
zilisema kuwa mchezaji huyo ambaye anatokea Zanzibar alitarajiwa kusaini
mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ya Jangwani.
“Anacheza namba sita uongozi ulimuona kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Burundi na kuvutiwa naye.
“Wamekuwa wakisema kuwa ndiye mbadala sahihi wa Frank Domayo ambaye ametimkia kwenye kikosi cha Azam FC.
“Uhakika ni kwamba jana usiku baada ya mechi kati ya Stars na Zimbabwe ndiyo walikuwa na mpango wa kumpa mkataba.
“Walimtumia mchezaji wao mmoja ambaye yupo Taifa Stars naye anatokea Zanzibar ndiye aliyefanya mipango yote,” kilisema chanzo hicho.