Mtabiri maarufu Bongo, Alhaji Maalim Hassan Yahya Hussein. Na Gladness Mallya na Deogratius Mongela Wakati Bunge la Bajeti 2014/15 li...
Na Gladness Mallya na Deogratius Mongela
Wakati Bunge la Bajeti 2014/15 likiendelea mjini Dodoma na hivi karibuni viongozi wa dini kutoa ufafanuzi wa kuonekana kwa mwezi mwekundu na kueleza kwamba unaashiria mwisho wa dunia, mtabiri maarufu Bongo, Alhaji Maalim Hassan Yahya Hussein amefunguka kwamba hiyo ni ishara kuwa, wabunge wengi watapoteza nyadhifa zao na viongozi wengi watakufa.

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Maalim Hassan alisema 
kuonekana kwa mwezi mwekundu (blood moon) Aprili 15, mwaka huu ni ishara
 kwamba viongozi wengi,  wakiwemo wa dini na serikali watakufa ghafla na
 wengine hasa wabunge watapoteza nyadhifa katika majimbo yao ya uchaguzi
 kutokana na sababu mbalimbali.
“Mwezi mwekundu ulioonekana ni dalili kwamba kutakuwa na habari 
nyingi za matatizo, njaa itakuwa kubwa, mashaka, uongo, viongozi 
kupingana huku wengine wakiondolewa madarakani kama wabunge au kufa 
ghafla.
“Kutatokea mizozo mingi kwa nchi ya Tanzania na nchi za jirani,” alisema Maalim Hussein.
Hata hivyo, mtabiri huyo aliwataka watu kuwa na tahadhari kwani Mungu anazungumza nao kwa ishara hizo zinazoonekana na mwezi utapatwa kwa mara ya pili na kuwa mwekundu Oktoba 23, mwaka huu, Jumanne ambayo kinyota ni siku ya mashaka.

GPL