Archive Pages Design$type=blogging

TABIA YA LULU KERO BONGO MUVI

WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kutojumuika na wenzake kwenye matukio ya kijamii hasa ...

WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kutojumuika na wenzake kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera Klabu ya Bongo Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria shughuli za wenziye kama misiba au hata sherehe zilianza tangu alipotoka gerezani Segerea, Dar.
Ilisemekana kwamba kilichosababisha viongozi wa Bongo Muvi kukasirishwa na kuamua kumweka kikao ili kumsema, ni kwamba ipo siku naye yatamfika.
Baada ya kuzinyaka ‘niuzi’ hizo motomoto, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo ili kumuonya kwa tabia yake hiyo kwa kuwa yeye bado mdogo.
Alisema Lulu anatakiwa afuate nyayo za wakubwa zake ambao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali kwa kuwa ipo siku naye yatamfika.
 “Lulu ni mtoto mdogo, hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda.
‘Lulu’ katika pozi tofauti.
“Sisi kama Bongo Movie tuna kawaida ya kuhudhuria shughuli za wenzetu pale inapobidi lakini kama mtu anakuwa na udhuru huwa anatoa taarifa lakini yeye hana kawaida hiyo, anajiona amekamilika.
“Naaamini ipo siku na yeye yatamfika kwa kuwa mitihani ni kawaida kwa binadamu, sidhani kama mtu atajitokeza na kumuunga mkono kwa tabia hiyo na siyo yeye tu anayejitenga, wapo na wengine wengi  lakini yeye bado ni mdogo kwetu huenda hajui alitendalo ndiyo maana tunataka tumfunze jinsi ya kuishi na watu,” alisema Steve.
Kwa upande wake Lulu alipotafutwa na kuulizwa juu ya jambo hilo hakuonesha mshtuko bali aliwaka: “Huyo aliyesema hivyo atajijua mwenyewe mimi sina shughuli na mtu, aachane na mimi.”

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: TABIA YA LULU KERO BONGO MUVI
TABIA YA LULU KERO BONGO MUVI
http://api.ning.com:80/files/Y4MVF3b94yIPDk6akdLf0*-Wp8MpOMkvS1vdil53o7v95UadbMzitTIx4FAn5m-wZ3pfd-CsFdqwE9TeFGlzB*AAzEuFauul/lulu1.png?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/05/tabia-ya-lulu-kero-bongo-muvi.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/05/tabia-ya-lulu-kero-bongo-muvi.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago