KAMATI ya Utendaji ya Simba, imeikataa ripoti ya kocha wao, Mcroatia, Zdravko Logarusic inayoonyesha ni wachezaji wangapi anataka kuw...

Logarusic amerejea kwao kwa ajili ya mapumziko baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika.
Hiyo ni siku chache tangu kamati hiyo kukutana kupitia ripoti ya usajili ya timu hiyo aliyoikabidhi hivi karibuni kabla ya kurejea kwao Croatia akisubiria mkataba mpya wa kuendelea kukinoa kikosi hicho kilichomaliza ligi kikiwa nafasi ya nne.
Kwa mujibu wa taarifa zilizofika kwenye meza ya Championi Jumatatu,
ripoti ya kocha huyo imewakataa wachezaji 17 kati ya 30 waliosajiliwa
msimu uliopita na inaonyesha kwamba kati ya hao, wanatakiwa wabaki 13
tu.
Hii ina maana kuwa Simba sasa watatakiwa kusajiliwa wachezaji wengine 17 kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya Logarusic, jambo ambalo kamati imelikataa.

Kamati hiyo imekataa kuwaondoa wachezaji wote hao kutokana na wengi
wao kubakiza mikataba ya mwaka mmoja, hivyo ili wasitishe mikataba yao
basi lazima wawalipe fedha.
“Tumeipitia vizuri ripoti ya kocha aliyoikabidhi kwenye kamati ya utendaji na kuona baadhi ya upungufu uliopo, hali inayotupa ugumu wa usajili kwa ajili ya msimu ujao.
“Ukiangalia ripoti hiyo inataka wachezaji 17 wasitishiwe mikataba yao kwa kile anachodai kuwa hawana uwezo wa kubaki kuendelea kuichezea Simba.
“Kati ya hao 17 basi ni watatu au wanne ambao wenyewe mikataba yao ndiyo imemalizika na hao wengine mikataba yao wamebakiza ya mwaka mmoja, hivyo kama kamati tunaona ni vyema tukawabakiza baadhi ya wachezaji kwa hofu ya kuingia hasara ya kulipa fedha nyingi kwa ajili ya kuvunja mikataba.
“Kwanza kuwasajili wachezaji 17 ili idadi kamili itimie litakuwa jambo gumu sana kwetu,” alisema mtoa taarifa huyo aliyekataa katakata kutajwa jina lake na Championi Jumatatu likaheshimu hilo.
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema: “Bado kamati ya utendaji na ya usajili zinaendelea kupitia ripoti ya mapendekezo ya kocha aliyoiacha, hivyo tusubirie mara baada ya kukamilika kila kitu kitawekwa wazi.”