Msanii wa muziki, Lady Jaydee leo amefikisha likes 300,000 kwenye mtandao wa Facebook na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufiki...
Msanii wa muziki, Lady Jaydee leo amefikisha likes 300,000
kwenye mtandao wa Facebook na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Tanzania
kufikisha idadi hiyo.
“Yoooooh!! Mmmefika laki tatu 300,000 na kuzidi, nawashukuru sana.
Fanyeni kubarikiwa leo, kesho, kesho kutwa na milele amina. Mapenzi tele
toka kwa JayDee,” ameandika.
Wasanii wengine wanaofuata nyuma yake kwa kuwa na likes nyingi kwenye
mtandao huo ni pamoja na Masanja Mkandanizaji, 208,053, Diamond Platnum
175,465 na Joti 158,919. Pia wapo wasanii wengine wengi ambao bado
akaunti zao zinakuwa taratibu.