Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema atajaribu kukaa na wasanii wa muziki Diamond na Ali Kiba ...
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph
Kusaga amesema atajaribu kukaa na wasanii wa muziki Diamond na Ali Kiba
na kuangalia tofauti zao ili kuwapatanisha.
Akizungumza na The Sporah Show hivi karibuni, Kusaga amedai kuwa
alikuwa hatambui kama wasanii hao wana matatizo kwenye kazi zao na
kuahidi kuwa ataliangalia tatizo lao.
“Kiukweli wote ni watoto wangu, Diamond ananipa heshima sana mimi
,namshukuru, Ali Kiba is the same, nafanya nao kazi na sijawahi
kugombana nao. Lakini sijui kama walikuwa wana tatizo ndo nasikia sasa,
lakini ngoja nijaribu kuwapigia ni find out kwanini? na kuna tatizo
gani between wao, lakini sijawahi kujua wana matatizo hayo.”