JAMANI mwishowe nitapasuka mdomo kwa kusema, mambo mengine kwa mwanamke aibu kuyafanya. Mnakuwa kama hamkwenda mkoleni mkafundwa mkafund...
JAMANI
mwishowe nitapasuka mdomo kwa kusema, mambo mengine kwa mwanamke aibu
kuyafanya. Mnakuwa kama hamkwenda mkoleni mkafundwa mkafundika. Hata
kama hukwenda bado una aibu ya kike, mnakimbilia mambo ya kuiga ndiyo
maana ndoa za siku hizi zimekosa neema wala maisha marefu.
Nani alikwambia kicheni pati ya siku moja unafunda mtu kama siyo
kukupoteza na kukupeleka siko. Si wajinga walianzisha mafunzo ya
mwanamke ya kuujua uanamke wake na thamani yake. Pia kujua mwanaume
umfanyie vitu gani apagawe na kuwaona wanawake wa nje si mali kitu.
Kujua viungo nyeti vya mwanamke viko wapi, anatakiwa avae nguo ipi
ili izibe sehemu gani, lakini leo hii kila mtu anajiendea bora liende,
mnatia aibu mbayaaa eeeeh.
Kweli sisi wanawake wa sasa hamnazo ili hali tunazo, tumekuwa kila
jambo tunaiga, jamani siyo kila kitu kipya lazima mwanamke akifanye au
akipate, wakati kila siku unaenda peke yako, huendi na mtu.
Leo nataka niwapashe tena wapashike, wanawake wasio na haya kufanya
mambo ya chumbani barabarani eti kwenda na wakati, wapiii?
Nimeshakueleza wakati hauendi na mtu, wewe tu na kujifanya unajua kumbe
unaungua na jua.
Jamani sasa hivi tembea barabarani utakutana na wanawake, vya siri
vimewekwa hadharani, maumbile yote ambayo hatakiwi kuyaona mtu zaidi ya
mwandani wako, imekuwa sasa hivi hayafichwi tena. Najiuliza hivi jamani
wanawake sasa hivi uanamke wetu hatuujui?
Kama inafika hatua unatembea na vazi linalomfanya mwanamke mwenzako
aone aibu, ujue umevuka ubinaadamu, sasa hivi ni mnyama kasoro mkia.
Sifa ya mnyama ni kufanya mambo bila kufikiri wala kuona aibu, ndiyo
maana mnyama anaweza kutembea na mama yake bila wasi na kumzalisha na
atakayezaliwa atatembea na bibi yake bila wasi!
Lakini kwa sisi wanadamu ukifanya hivyo litakuwa gumzo la mwaka na kila mmoja atakulaani.
Sasa hivi mjini hajulikani nani changu nani mke wa mtu wala nani yupo kwa wazazi wake.
Sasa hivi mjini hajulikani nani changu nani mke wa mtu wala nani yupo kwa wazazi wake.
Ni vululuvululu, mavazi wanayovaa machangu usiku kutafutia wateja
ndiyo mavazi ya wasichana na kina mama mchana, mbona aibu. Jamani tatizo
nini kufikia hatua ya kugeuka mahayawani na akili tunazo!
Nani aliyekuambia sifa ya mwanamke kwa mwanaume ni kutembea kwa
kuyaacha maumbile nyeti kila mtu ayaone, bila kujali anayeona ni mtoto
mdogo au mzee. Sasa hivi kuziona shanga, nguo za ndani ni jambo la
kawaida hata matiti nje!
Mmh! Kweli kazi ipo wazazi wana kazi ya ziada kwa watoto wa kike.
Ndani ya daladala unamkuta mtu kavaa suruali isiyo na mkanda ndani kavaa
bikini na anaimana bila wasiwasi. Unajiuliza mtu huyo na mbuzi wana
tofauti gani!
Huenda mnaamini kufanya hivyo ndiyo njia ya kumnasa mwanaume, basi
mnajidanganya. Muoaji hawezi kukuchukua kwa kuamini wewe si mwanamke
sahihi baada ya kuuona mwili wako hatakuwa na kitu anachokitaka zaidi ya
kuyatamani maumbile yako kisha kufanya mapenzi na wewe na kukuacha.
Kwa mtindo huu wa kutembea uchi mkidhani ndiyo njia ya kumpata
mwanaume mtakuwa mnajidanganya zaidi ya kugeuzwa Big G utatafunwa na
kutemwa.
Hata kama ukiwa mtaalamu wa mapenzi, huwezi kuolewa zaidi ya watu
kubadilishana na kukuacha akionekana huna maana na kuwa jamvi la wageni.
Ndiyo maana kuna wasichana wazuri wenye sifa lakini mpaka leo hawaolewi
kutokana na kuwa na sifa mbaya.
Jamani si kila biashara inataka matangazo, mengine ni kujidhalilisha.
Hebu badilikeni, yafunikeni maumbile yenu ili wanaume wavutike kuwaoa, mwanaume pamoja na kupenda umbile zuri lakini kikubwa wanaangalia sana tabia. Kwa leo yanatosha tukutane wiki ijayo.
Hebu badilikeni, yafunikeni maumbile yenu ili wanaume wavutike kuwaoa, mwanaume pamoja na kupenda umbile zuri lakini kikubwa wanaangalia sana tabia. Kwa leo yanatosha tukutane wiki ijayo.
Ni mimi anti Nasra Shangingi Mstaafu.
- GPL