MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa ...
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Wolper alisema anaamini serikali ya tatu itakuwa mzigo kwa wananchi ambao ndiyo walipa kodi. MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali mbili na si tatu wala ya mkataba.
Muigizaji staa Bongo, Jacqueline Wolper
“Serikali mbili ndiyo mpango mzima, ya tatu ni mzigo, ya mkataba
sioni maana yake. Halafu nataka muungano udumu, pia nitafurahi sana kama
Ukawa watarudi bungeni litakapoanza tena Agosti mwaka huu,” alisema
Wolper.