INASIKITISHA! Tofauti na makaburi mengine ya wasanii mbalimbali wa filamu yaliyopo...
INASIKITISHA! Tofauti na
makaburi mengine ya wasanii mbalimbali wa filamu yaliyopo Kinondoni
jijini Dar, la marehemu Adam Kuambiana limeendelea kubomoka na kuwa na
mashimo huku likionekana kutelekezwa.
Akizungumza msanii mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema wasanii ambao walikuwa wakifanya kazi na marehemu hawafanyi vizuri kwani wana uwezo wa kujichangisha na kulijenga kaburi hilo kama alivyofanya Jeniffer Kyaka ‘Odama’ alivyotoa mchango mkubwa kulijengea kaburi la Recho.