Muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sep...
Muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa
karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu amezungumzia kauli ya
Diamond aliyotoa hivi karibuni kuwa mpenzi wake ana marafiki wapenda
starehe na anasa.
Aunt amesema kuwa Wema ni mtu mzima anajua baya na jema.
0
“Diamond alivyoongea pale hakunitaja jina, kwahiyo nikisema kwamba
aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo. Yeye aliongea kwa niaba ya
watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitaja jina sidhani kama
angeongea kwamba yule mtu anafundishwa,” amesema Aunt. “Wema ni mtu
mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa
kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna
wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda
wangu wa kazi na nina muda wangu waku spend.”
“Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti
nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya
kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema
nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika
kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya
Diamond.”
Kwa upande mwingine muigizaji huyo amesema anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Mwajuma Nipe’.