Bila shaka umeshakutana na tweets au picha kwenye Instagram inayoonesha upigaji kura wa tuzo za BET ambapo kwenye kipengele cha Best Int...
Bila shaka umeshakutana na tweets au picha kwenye Instagram
inayoonesha upigaji kura wa tuzo za BET ambapo kwenye kipengele cha Best
International Act: Africa, Diamond anaonekana kuongoza. Well, ni good
news kwa mashabiki wake lakini bad news ni kuwa kura hizo hazihusiki
kabisa na kura zenyewe za BET kumpata mshindi.
Kituo cha redio cha V101.9 cha Marekani kimetengeneza utaratibu wake mwenyewe
wa kuwapa nafasi wasikilizaji na wasomaji wake kumpigia kura msanii
wanayempenda na kura hizo zitaishia kuwapa wao picha ya namna wasomaji
wanapendekeza washindi wao. Kufanya hivyo ni rahisi sana na hata sisi
tukiamua kutengeneza ballots systems kama hizi ingewezekana.
Utaratibu wa tuzo za BET upo tofauti kabisa na unaotumika kwenye tuzo
zingine kama CHOAMVA ama MTV MAMA ambapo baada ya majina kutangazwa,
mashabiki huwapigia kura wasanii wanaowapenda.
Kwenye tuzo za BET kuna jopo ama academy maalum yenye watu takriban
500 ambao ni wadau wa kiwanda cha muziki, habari na bloggers. BET
huwataka watu hawa kupendekeza majina kwenye kila kipengele kwa mfumo
wa kupiga kura ‘electronically’.
Kura hizi husimamiwa na kundi liitwalo “Yangaroo”
ambalo hufanya kazi kwenye tuzo zingine pia. Kundi hili hupunguza
majina na kubakiza wasanii watano kwenye kila kipengele na kuyatuma tena
majina hayo (ambayo hutagazwa sasa rasmi kama majina ya mwaka husika)
na kuyarudisha tena kwenye academy hiyo itakayopiga kura za mwisho
kupata mshindi.
Habari njema ni kuwa, Vanessa Mdee pia ni miongoni mwa member wa
academy hiyo. Hivyo bila wasiwasi atampigia Diamond. Haijulikani kuna
members wangapi Afrika Mashariki ambao kiuzalendo watatakiwa kumpigia
kura Diamond.